HALI
ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini si
ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji
Kutokana
na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio
Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili
ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa
Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa
wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka
sasa
Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania
wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu
za matibabu zifwatwe
"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri
anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado
hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa
ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud
Aliongezea kuwa kwa
upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa
ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini
Matumaini
ni msanii kwenye upande wa uchekeshaji. alianza kazi hiyo katika kundi
la Kaole na kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie Kiwewe
No comments:
Post a Comment