MSANII anayeshikilia soko la filamu kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza scenes za mapenzi na hata zile za kijamii, Irene Uwoya, amedai mashabiki wake wengi wanamtaka acheze filamu moja na hasimu wake mkubwa Jackline Wolper,
ila moyo wake haupo tayari kwani anaamini msanii huyo kiwango chake ni
kidogo hivyo kwenye filamu anaweza kumtia hasara ya sokoni.
Mwandishi
wahabari hii alipotaka kujua ni lini watakuja kushiriki filamu ya
pamoja ili kuwaonesha mashabiki wao viwango vyao, ndipo alipoamua kutoa
kauli hiyo kuwa kiwango chake ni kikubwa na hakuna asiyejua hilo hivyo
akishiriki kazi moja msanii huyo wote wanaweza kuonekana chipukizi kwani
filamu inaweza kuwa mbaya kuliko maelezo.
“Nadahani unajua
mimi na huyo msanii tukoje hivyo sidhani kama naweza kushiriki kwenye
filamu yake au yangu kwa sababu najua kiwango chake ni kidogo mno,
ingawa sisemi kwamba hajui kuigiza ila bado hajafikia mziki huu,” alidai Uwoya.
Hata
hivyo Wolper alipotafutwa ili kuongelea kiwango anachosema Uwoya
hakuweza kupatikana na hadi kazi hii inaenda mitamboni simu yake ilikuwa
haipatikani.
No comments:
Post a Comment