Tuesday, September 18, 2012

Baby Madaha kumuiga Rihanna

MSANII anayefanya poa kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amefunguka kuwa anazimika na swaga za mwanamuziki kutoka Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’ hadi kufikia hatua ya kumuiga swaga zake.

Akizungumza na Mbovu Mbovu za Mastaa, amejikuta akifanya kila kitu anachokifanya mwanamuziki huyo kutokana na mapenzi aliyonayo kuanzia mavazi, kuimba na hata kucheza.

“Kiukweli huwa najikuta nikifanya vitu kama vya Rihanna na sijui kwa nini kwa sababu awali haikuwa hivi lakini sasa kila kitu anachokifanya Rihanna basi utakuta na mimi nakifanya,” alisema Baby Madaha.…

No comments:

Post a Comment