Wednesday, September 19, 2012

Baada ya Yna sasa mjue JERICHO ROSALES/ANGELLO




                                       Jericho na Kim katika pozi

Jericho Vivar Rosales (amezaliwa tar. 22 Septemba, 1979 mjini Quezon, Ufilipino) ni mwigizaji wa kifilipino. Alianza kazi ya uigizaji baada ya kushinda katika mashindano ya Mr. Pogi (mashindano ya Urembo yanayohusisha wanaume) mwaka 1996. Echo, kama anavyojulikana na wengi, ameumbwa na vipaji vingi.Yeye ni muigizaji, muimbaji, mtunzi wa nyimbo, mchezaji(mnenguaji) na muongozaji(aliongoza video za nyimbo mbili na alishirikiana kuongoza na Gary Valenciano katika matamasha yake ya Music Music hapo Oktoba 18 mpaka 19, 2007).
Echo alijiunga Star Circle mnamo 1997. Katika maonesho madogo, Alishiriki katika tamthilia kama Maalaala Mo Kaya, Pangako sa Yo, Sana'y Wala Nang Wakas na Ang Panday. Tamthilia ya Pangako sa Yo ilimfanya kuwa maarufu mno sio tu Phillipines bali hata katika mataifa ya Kusini-Mashariki Mwa Asia kama vile Malaysia.
Rosales alishiriki kama nyota katika filamu mahiri za Tanging Yaman, Baging Buwan, Noon at Ngayon, Santa Santita na Nsaan Ka Man. Yeye pia alishirikishwa katika timu ya wapenzi pamoja na Kristine Hermosa katika filamu za Trip, Forevermore, na Ngayong Nandito Ka. Filamu yake ya hivi karibuni ililenga maisha halisi ya Mwanandondi maarufu wa Ufilipino, Manny Pacquiao.
Mnaomo mwezi Machi mwaka 2006, EMI Malaysia walisaini na Rosales na Bendi yake ya Jeans (yeye ni mwimbaji kiongozi na mtunzi wa karibu nyimbo zote za hiyo bendi) album yao ya kwanza iliitwa Loose Fit.
                                                KIM JONES
                                 Jericho akijivinjari na Kim Jones
                                        Jericho akiwa na X girlfriend wake Heart Evangalista

         Mnamo 14 mwezi wa nne mwaka huu Jericho maarufu kama Angello ameweka wazi mahusiano yake na mtangazaji wa television  KIM JONES {pichani juu}kwa sasa ndo mpenzi wake baada ya kuachana na muigizaji mwenzake HEART EVANGALISTA na wote wamekili kupendana sana baada ya kuhojiwa na mtandao wa ABS-CBN NEWS.

No comments:

Post a Comment