Saturday, January 19, 2013

WANAPIGA MZIGO... BILA MBWEMBWE

RUTH SUKA ‘MAINDA’ Mainda ni zao la Kundi la Maigizo la Kaole, mara nyingi huwa haonekani. Anapenda kufanya mambo yake kwa vitendo bila mbwembwe. Filamu zake ni nzuri, ana uwezo mkubwa wa kuigiza.

SALOME MISAYO ‘THEA’
Kabla hajaolewa, kidogo alikuwa akionekana japo si sana. Alipoolewa ndiyo kabisa. Zaidi utamuona pindi wanapokuwa ‘location’ au kwenye tukio muhimu linalohusishaa wasanii kwa jumla.

BLANDINA CHAGULA
‘JOHARI’ Unaweza kusema amesafiri au hayupo nchini kumbe amejichimbia katika kampuni yao ya RJ na mkurugenzi mwenza, Vincent Kigosi ‘Ray’ wanazitengeneza filamu zao kimyakimya. Mara nyingi unaweza kumuona Ray katika filamu au viwanja vya bata lakini Johari ni nadra sana.

YVONNE-CHERRY
NGATIKWA ‘MONALISA’
Mama yake ni mwigizaji na yeye pia, amefuata nyayo. Mara nyingi unaweza kusema hayupo nchini lakini ukweli ni kwamba anapiga mzigo katika levo za kimataifa na ana bidii ya kukua kila siku.

SABRINA RUPIA ‘CATHY’
Mama mwenye familia, anaigiza filamu zake huku akiwa mjasiriamali. Ukimtazama unaweza kusema haigizi lakini ukweli ni kwamba yupo ndani ya gemu kitambo toka Kundi la Sanaa la Mambo Hayo lililokuwa likirusha michezo yake runingani kabla halijafa.

WASTARA Safari yake kwenye soko la filamu iligubikwa na changamoto nyingi, hakukata tamaa. Anapokuwa mzigoni huwa hapendi kujionesha, hufanya kwa vitendo zaidi. Kazi zake zinaonekana.

ISSA MUSSA ‘CLOUD 112’ Ni miongoni mwa wasanii ambao mara nyingi hawapendi kujionesha katika vyombo vya habari. Filamu zake ni nyingi na mafanikio yake ni makubwa, zinapendwa na watu wengi.

JACOB STEVEN JB: Anapiga mzigo chini ya kampuni yake ya Jerusalemu Film Company. Staili yake ya maisha unaweza kusema hayupo vile, asikwambie mtu jamaa anapiga mzigo, anakubalika na aliwahi kushinda tuzo za Ziff katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume mwaka 2011.
Idadi ya wasanii wanaofanya kazi zao bila mbwembwe ni kubwa lakini kutokana na uhaba wa nafasi hawa wanawawakilisha wenzao.

No comments:

Post a Comment